Hotline +255 768985500

Whistleblowing

Benki ya Equity Tanzania imezindua rasmi Zanzibar Supreme, kituo cha huduma maalum za Equity bank kinacholenga kutoa huduma za kifedha zenye uzoefu wa hali ya juu, ushauri wa kibiashara na mahusiano ya karibu na wateja, kinachopatikana Kijangwani, Mjini Magharibi Zanzibar. Hii ikiwa ni hatua muhimu katika mkakati wa benki hiyo wa kuimarisha huduma za kifedha, kupanua ujumuishaji wa kifedha na kusaidia ukuaji jumuishi wa uchumi wa Zanzibar.






Naibu Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dkt. Hamad Omar Bakari (katikati) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Isabela Maganga (watatu kushoto) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ali Maulid Juma wakizindua Kituo Kipya cha Zanzibar Suprime cha Benki ya Equity Tanzania, kilichopo eneo la Kijangwani, Zanzibar, Juni 6, 2026. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Equity, Prosper Nambaya, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Dkt. Said Haji Mrisho, Mteja wa Benki ya Equity, Dkt. Issa Seif Pamoja na Meneja wa Kituo cha Zanzibar Suprime, Anas Ramadhan.



Uzinduzi wa Kituo cha Zanzibar Supreme unaongeza imani kwenye benki hiyo katika fursa za ukuaji wa uchumi wa Zanzibar pamoja na dhamira yake ya kuendelea kuhudumia wananchi, wafanyabiashara, taasisi na wawekezaji kwa karibu zaidi. Uzinduzi huu wa kituo cha Zanzibar Supreme uliongozwa na Mh. Dr. Hamad Omar Bakar, Naibu waziri wa Fedha na Mipango ambaye alikua ni Mgeni rasmi.







Kituo cha Zanzibar Supreme kimeanzishwa kwa lengo la kuhudumia wateja wa hadhi ya juu, wajasiriamali wakati na wa kubwa, kampuni, sekta ya hoteli, wawekezaji, pamoja na wadau wengine muhimu kupitia huduma za kibenki za kiwango cha juu, zenye kuzingatia mahitaji ya mteja na uhusiano wa karibu kati ya benki na mteja.






Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Bi. Isabela Maganga, alisema kufunguliwa kwa kituo hiki ni sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo wa kuwekeza katika huduma za kibenki zinazogusa sekta muhimu za uchumi na kuongeza upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha.




“Uzinduzi wa kituo cha Zanzibar Supreme ni hatua muhimu katika safari yetu ya kuendelea kusogeza huduma za kifedha karibu na wateja wetu. Kupitia kituo hiki, tunalenga kutoa huduma za kibenki zinazokidhi mahitaji ya wateja binafsi, wafanyabiashara wa kati na wakubwa, kampuni, wawekezaji na sekta ya hoteli, ambayo ni moja ya nguzo muhimu za uchumi wa Zanzibar,” alisema Bi. Maganga. Aliongeza kuwa Equity Bank Tanzania itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya vituo vya hudum kwa wateja, huduma za kidijitali, na suluhisho za kifedha zinazosaidia ukuaji wa biashara, uwekezaji, upatikanaji wa mitaji, na uwezeshaji wa kifedha wa muda mrefu. “Tunaamini kuwa taasisi za fedha zina jukumu muhimu katika kusaidia maendeleo ya kiuchumi kwa kutoa huduma zinazowezesha watu na biashara kushiriki kikamilifu katika uchumi rasmi. Kituo hiki ni sehemu ya dhamira yetu ya kusaidia ukuaji wa Zanzibar kupitia huduma bora, za kuaminika na zinazolenga mahitaji halisi ya wateja,” aliongeza uzinduzi huu pia unaendana na jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, za kuendeleza ukuaji endelevu wa kijamii na kiuchumi, kuongeza ushiriki wa wananchi na sekta binafsi katika uchumi, na kuwezesha mabadiliko chanya katika sekta za fedha na biashara kwa mwaka 2026 na kuendelea. Kituo cha Zanzibar Supreme kitatoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo kufungua akaunti, huduma za mikopo, huduma za biashara, huduma za fedha za kimataifa, huduma za kidijitali, ushauri wa kifedha, na huduma mahsusi kwa wateja wanaohitaji uangalizi wa karibu na suluhisho za kifedha zilizoboreshwa. Hafla ya uzinduzi wa kituo hiki umewakutanisha viongozi wa Serikali, viongozi wa taasisi mbalimbali, wamiliki na watendaji wa hoteli, wafanyabiashara wakati na wakubwa, wawekezaji, wateja wa kimkakati na wadau wengine muhimu kutoka Zanzibar. Kwa kufunguliwa kwa Zanzibar Supreme, Equity Bank Tanzania sasa ina jumla ya matawi 19 nchini, hatua inayozidi kuimarisha uwepo wake na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha katika maeneo muhimu ya kibiashara na ukuaji wa uchumi. Mtandao wa matawi ya Benki unajumuisha Makao makuu / Golden Branch, Golden Supreme, Quality Centre, Kariakoo, Mwenge, Ubungo, Mbagala, Temeke na Nyerere jijini Dar es Salaam, pamoja na matawi yaliyopo Arusha, Mwanza, Dodoma, Moshi, Mbeya, Morogoro, Geita, Kahama na Zanzibar, ikiwemo kituo cha Zanzibar Supreme kilichozinduliwa rasmi.









Related stories

Equity Bank Tanzania limited imeingia ubia na Klabu ya Simba

Equity Bank Tanzania limited imeingia ubia na Klabu ya Simba katika kutoa kadi zenye chapa zao...

View More
Equity Bank Kicks Off Issuance of Simba Fan Cards

Equity Bank has today kicked off the issuance of Simba Fan Cards to over 20 million fans of the...

View More
Equity Bank Tanzania Donates 5 Mobile Police Posts to Ministry of Home Affairs in Tanzania

Equity Bank Tanzania has today handed over 5 mobile police posts to the Ministry of Home Affairs...

View More
Benki Ya Equity Tanzania Inazindua Suluhisho Jipya Ya Benki Kimtandao

Benki ya Equity imezindua huduma za benki kwa njia ya kimtandao, huduma hizi zilizopewa jina...

View More
Equity Bank and Tanzania Revenue Authority in Partnership for Payment of Taxes

The new tax settlement avenue will be available for all TRA clients including non- Equity Bank...

View More
Equity Bank Group Third Quarter Profits Soars 26% on the Back of Growing Regional Economic Activities

Equity Bank Group, on Thursday announced that its profit after tax for the third quarter of 2014...

View More
Regional Expansion and Diversification Strategy Pays Off as Equity Bank Posts a 21% Growth

Regional financial services provider Equity Bank Group has returned to its traditional growth path...

View More
Equity Bank Group’s Investment in Ict and Focus on Sme Boosts Profits by 11% in the 2013

Equity Bank Group’s investment in ICT and Focus on SME boosts profits by 11 percent in the year...

View More
Equity Bank and American Express Announce Card Issuing and Merchant Acquiring Partnership

Equity Bank and American Express today announced a partnership agreement, through which Equity Bank...

View More
Equity Group Secures Its Shareholders Nod for a Kshs 20 Billion Pan African Expansion Bid

The approvals, which were secured during the firm’s 11th Annual General Meeting (AGM) held today...

View More
Equity Bank’s Focus on Innovation Boosts First Half Year 2013 Profit

Regional banking group, Equity Bank's reduction of interest rates by 700 bps from 25% to 18% has...

View More
Equity Bank Group Strengthens Its Fundamentals While Expenses of Ict, Innovation and Product Rollout Slows Profit Growth To 7%

Equity Bank Group strengthens its fundamentals while expenses of ICT, Innovation and Product Rollout...

View More
Equity Bank's Strategy Increases Profits by 36 Percent

The Group’s total assets posted a 24% growth during the year to close at Ksh 243 billion up from...

View More
MasterCard and Equity Bank Announce Partnership to Introduce PayPass™ Enabled Cards

Partnership to increase financial inclusion and boost EMV migration efforts in the region.

View More
Equity Tanzania unveils a new identity in line with the Bank’s ongoing journey of transformation

The new identity is aimed at creating a sustainable growth path and service delivery in today’s...

View More
Equity ranks position 7 in the list of top 10 banks in Africa in The Banker’s Top 100 African Banks 2020.

Equity becomes the 1st bank in Eastern and Central Africa to achieve this milestone paving way for...

View More
EQUITY CROSSES THE KSH 1,000,000,000,000 BALANCE SHEET MARK

Becomes the first bank in Eastern and Central Africa to achieve the trillion-shilling balance sheet...

View More
Equity CEO, Dr. James Mwangi, wins coveted Oslo Business for Peace Award

The Award is conferred annually to exceptional individuals who exemplify their outstanding `business...

View More
EQUITY BANK (T) ANNOUNCES PARTNERSHIP WITH WORLD REMIT, MONEY GRAM AND WESTERN UNION TO EASE INTERNATIONAL MONEY TRANSFERS TO TANZANIA

The service presents the exciting prospect for the Tanzania community to receive seamless...

View More
EQUITY BANK (T) LTD YAZINDUA KAMPENI MPYA YA KUWEKA AKIBA (JIJENGE)

Equity Bank (T) leo imenzidua rasmi akaunti maalum ya utunzani fedha kwa kujiwekea kidogo kidogo ili...

Zaidi
EQUITY BANK (T) yaleta mfumo wa kidijitali wa “Eazzy-Kikundi” ili kuongeza tija na uwazi katika uendeshaji wa Vicoba nchini.

Equity Bank (T) imeahidi kuendelea kutoa elimu ya fedha na mikopo nafuu kwa vikundi vya uwekezaji na...

Zaidi
Equity Bank (T) introduces Interbank money transfers and SADC-(SIRESS) Services to boost cross boarders' and regional remittance services

Customers with Equity Bank accounts can now transact seamlessly in any of the Equity Bank branches...

View More
Equity Bank launches EazzyFX, An Electronic Channel for Settling Forex Transactions

Customers will have the freedom to execute forex requirements in real-time in a safe, convenient and...

View More
Equity receives double International Standards Certification on IT Service and Information Security Management Systems

Equity Bank Kenya Limited has received two International Standards Certifications - ISO 20000 and...

View More
Equity Bank Tanzania Limited Appoints Managing Director

Equity Bank Tanzania has announced the appointment of Ms. Isabel Maganga as the new Managing...

View More
Equity Group Launches Kshs. 678 billion (USD 6 Billion) Regional Private Sector Economic Recovery and Resilience Stimulus Plan

Equity’s Eastern and Central Africa Recovery and Resilience plan is envisaged to provide financing...

View More
Equity Group Returns to Growth

Equity Group has eased its defensive strategy that had been deployed during the economic uncertainty...

View More
THE AFRICAN CONTINENTAL FREE TRADE AREA (AfCFTA) SECRETARIAT AND EQUITY GROUP CEMENT A PARTNERSHIP TO DEEPEN ECONOMIC INTEGRATION OF THE AFRICAN CONTINENT

The partnership will champion the implementation of the Africa Recovery and Resilience Plan which...

View More
EQUITY BANK TANZANIA HOSTS AMERICAN DELEGATES FOR A TRADE AND INVESTMENT TRADE MISSION

Delegates from the United States of America (USA) have arrived in Dar es Salaam, Tanzania for a...

View More
EQUITY GROUP REPORTS STRONG 3RD QUARTER PERFORMANCE

Equity Group Holdings Plc today reported Kshs.34.4 billion shillings profit after tax for the nine...

View More
EQUITY GROUP REPORTS A RECORD KES 46.1B NET PROFIT AND A DIVIDEND PAYOUT OF KES 15.1B

EQUITY GROUP REPORTS A RECORD KES 46.1B NET PROFIT AND A DIVIDEND PAYOUT OF KES 15.1B

View More
Equity Group Holdings Registers Strong Recovery

Nairobi Monday 13th May 2024… After reporting a 5% decline in profit after tax for the year ended...

Read More
Equity Group Unveils 2023 Sustainability Report: “A Sustainable World is a Transformed Africa” Showcasing Bold Vision and Impact

Nairobi, Kenya, 3rd September 2024: Equity Group unveiled its third annual sustainability report for...

Read More
Equity Group Holdings Plc Reports 3rd Quarter 2024 Profit After Tax of Kshs 40.9 Billion

NAIROBI, 12th November 2024: Against a backdrop of continued macroeconomic headwinds of high...

Read More
Equity Group Reports Kshs 60.7 Billion Profits Before Tax, Driven by Strategic Diversified Growth

NAIROBI, 27th March 2025: Equity Group Holdings Plc continues to deliver solid financial results,...

Read More
Equity Group Reports Kshs 15.4 Billion Profits After Tax on Prudent Cost Management and Resumption of Growth

NAIROBI, 29th May 2025: Demonstrating strategic agility and resilience in a dynamic global economic...

Read More
Equity Group Announces Strong Q3 2025 Results, Recording a 32% Growth in Profit After Tax Reflecting Strategic Transformation

Equity Group Holdings Plc has announced its Q3 2025 results, showcasing a robust performance driven...

Read More
Equity Bank Tanzania Launches "Ushonaji Plus" An Asset Loan for Tailoring Equipment Aimed at Supporting Women Entrepreneurs in the Tailoring and Fashion Design Sector.

Asset Loan to Empower Women and Youth Entrepreneurs in Tailoring and Fashion Design Sector

Read More
Benki ya Equity tanzania yakabidhi vifaa vya kuhifadhi taka katika soko la samaki la mwaloni na kufanya usafi kwenye ufukwe wa ziwa victoria, jijini mwanza.

Mwanza, Tanzania –Tarehe 24 Januari 2026. Benki ya Equity Tanzania, kwa ushirikiano na wadau...

Read More
Benki ya Equity yazindua “wezesha account” akaunti ya amana ya muda maalum, inayolenga kuimarisha uwekezaji na uwezeshaji wa kifedha.

Benki ya Equity yazindua “wezesha account” akaunti ya amana ya muda maalum, inayolenga...

Learn More
BENKI YA EQUITY NA MIXX BY YAS WAINGIA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KUPANUA WIGO HUDUMA ZA KIFEDHA KUPITIA MAWAKALA NCHINI TANZANIA

Tanzania, Benki ya Equity imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Mixx by Yas wenye lengo la kuleta...

Read More
Equity Bank Tanzania Yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa Kuwawezesha Wanawake.

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Equity Bank Tanzania iliwaunganisha wanawake wateja na...

Read More
BENKI YA EQUITY TANZANIA YAZINDUA TAWI JIPYA LA UBUNGO LILILOPO EAST AFRICAN COMMERCIAL LOGISTICS CENTRE (EACLC MALL) JIJINI DAR ES SALAAM.

Benki ya Equity Tanzania imezindua rasmi tawi jipya la Ubungo, lililopo ndani ya EACLC Mall (East...

Read More
Service finder
Equity Bank is Regulated by Bank of Tanzania (BOT)