Hotline +255 768985500
Hotline +255 768985500
Tanzania, Benki ya Equity imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Mixx by Yas wenye lengo la kuleta huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi kupitia mtandao mpana wa mawakala wa Mixx by Yas waliopo nchi nzima. Ushirikiano huu unaimarisha juhudi za benki katika kupanua ujumuishaji wa huduma za kifedha kwa kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa haraka, rahisi na kwa kuaminika popote walipo, mijini na vijijini.
Kupitia ushirikiano huu, wateja wa Benki ya Equity sasa wanaweza kupata huduma za kifedha moja kwa moja ikijumuisha kuweka pesa kwenye akaunti zao za Equity, na kutoa pesa ili kufanya matumizi mbali mbali, sasa wataweza kufanya hivyo kupitia mawakala wa Mixx by Yas waliopo Tanzania nzima. Wateja wa Benki ya Equity wenye simu janja wanaweza kutumia Equity Mobile App kufanya miamala hii, huku wanaotumia simu za kawaida wakipata huduma kupitia USSD code *150*07#. Njia hizi zinawawezesha kufanya miamala ya Kuweka na Kutoa fedha kwa urahisi, kwa haraka na kwa usalama kupitia mawakala walioko karibu nao, huku ikibebwa na kauli mbiu: Equity Bank “Weka Pesa, Toa Pesa.” Na Mixx By Yas
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Bi. Isabela Maganga, alisema:
“Ushirikiano huu na Mixx by Yas una thamani ya kimkakati inayokwenda mbali zaidi ya utoaji wa huduma za kibenki, ni hatua mahsusi ya kuboresha huduma zetu kwa kuwafikia kiurahisi, kupunguza umbali kati ya wateja na huduma za kibenki, kwa kuwaletea huduma karibu na maeneo wanayoishi na kufanyia kazi. Kupitia mtandao mpana wa mawakala wa Mixx by Yas, waliopo Tanzania nzima, wateja sasa hawatalazimika kusafiri umbali mrefu kufika matawi yetu ya benki, bali wanaweza kupata huduma ya Kuweka Pesa kwenye akaunti zao, na Kutoa Pesa kwa matumizi mbali mbali kwa urahisi, gharama nafuu na usalama mkubwa kupitia mawakala wa Mixx by Yas wanaowaamini karibu yao.
Kwa wateja wa Benki ya Equity, ushirikiano huu unamaanisha upatikanaji wa huduma za kifedha zilizo karibu, rahisi na za kuaminika. Kwa mawakala wa Mixx by Yas, unafungua fursa za kiuchumi kupitia ongezeko la miamala, wigo mpana wa huduma na ukuaji wa biashara zao. Na kwa jamii kwa ujumla, tunachochea ujumuishaji wa kifedha, tunaimarisha mzunguko wa fedha katika uchumi wa ndani na kusaidia wananchi kushiriki kikamilifu katika mfumo rasmi wa kifedha.
Tunawaalika wadau wote kuupokea na kuutumia ushirikiano huu kwa sababu unaweka msingi wa mfumo wa kifedha ulio karibu na watu, unaoaminika na unaochochea maendeleo. Maono yetu ni kufanya huduma za kibenki ziwe sehemu ya maisha ya kila siku, na hatua hii ni muhimu katika kufanikisha dhamira hiyo.
Kwa upande wake, Angeliqa Pesha, CEO wa Mixx by Yas, alisema,”Kwa kuunganisha uzoefu wa kibenki wa Equity na nguvu ya jukwaa la Mixx pamoja na mtandao mpana wa mawakala wetu, tunabadilisha vituo vya huduma vilivyo karibu na jamii kuwa milango kamili ya huduma za kibenki. Kupitia ushirikiano huu, ikiwemo upanuzi wa huduma za utoaji wa fedha za kimataifa (IMT), tunaongeza upatikanaji, urahisi na uaminifu kwa mamilioni ya Watanzania. Kwa pamoja, tunajenga mfumo wa kifedha ulio jumuishi zaidi, unaounganishwa kidijitali na wenye kuwezesha uchumi wa taifa.”
Ushirikiano kati ya Benki ya Equity na Mixx by Yas unaakisi mwelekeo wa sekta ya kifedha wa kuunganisha na kuwafikia wateja kwa ukaribu zaidii. Kwa kutumia mawakala wa Mixx by Yas ambao wanaaminika na jamii, huduma za kibenki za Equity sasa zinapatikana karibu zaidi na wananchi kuliko wakati wowote.
Mbali na mkakati huu huu wa kusogeza huduma kwa wateja, Benki ya Equity inaendelea kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja wake. Hivi karibuni benki imezindua Wezesha Account, Akaunti ya Amana ambayo ni suluhisho la uwekezaji wa muda mfupi inayowapa wateja faida kubwa ya uwekezaji, kwa kianzio ni TZS. 500,000 tu, kwa muda wa miaka mitatu (3). Aidha, kupitia akaunti ya Amana ya Muda wateja wanaweza kukopa hadi asilimia 80 ya akiba yao bila kuvunja amana. Ubunifu huu unaonesha dhamira ya benki ya kuendeleza ujumuishaji wa kifedha na kujenga jamii zilizo imara zaidi kiuchumi.
Kwa maelezo zaidi:
Tembelea tawi la karibu la Benki ya Equity, piga simu 0768 985 500, tuma barua pepe info@equitybank.co.tz.



Equity Bank Tanzania limited imeingia ubia na Klabu ya Simba katika kutoa kadi zenye chapa zao...
View MoreEquity Bank has today kicked off the issuance of Simba Fan Cards to over 20 million fans of the...
View MoreEquity Bank Tanzania has today handed over 5 mobile police posts to the Ministry of Home Affairs...
View MoreBenki ya Equity imezindua huduma za benki kwa njia ya kimtandao, huduma hizi zilizopewa jina...
View MoreThe new tax settlement avenue will be available for all TRA clients including non- Equity Bank...
View MoreEquity Bank Group, on Thursday announced that its profit after tax for the third quarter of 2014...
View MoreRegional financial services provider Equity Bank Group has returned to its traditional growth path...
View MoreEquity Bank Group’s investment in ICT and Focus on SME boosts profits by 11 percent in the year...
View MoreEquity Bank and American Express today announced a partnership agreement, through which Equity Bank...
View MoreThe approvals, which were secured during the firm’s 11th Annual General Meeting (AGM) held today...
View MoreRegional banking group, Equity Bank's reduction of interest rates by 700 bps from 25% to 18% has...
View MoreEquity Bank Group strengthens its fundamentals while expenses of ICT, Innovation and Product Rollout...
View MoreThe Group’s total assets posted a 24% growth during the year to close at Ksh 243 billion up from...
View MorePartnership to increase financial inclusion and boost EMV migration efforts in the region.
View MoreThe new identity is aimed at creating a sustainable growth path and service delivery in today’s...
View MoreEquity becomes the 1st bank in Eastern and Central Africa to achieve this milestone paving way for...
View MoreBecomes the first bank in Eastern and Central Africa to achieve the trillion-shilling balance sheet...
View MoreThe Award is conferred annually to exceptional individuals who exemplify their outstanding `business...
View MoreThe service presents the exciting prospect for the Tanzania community to receive seamless...
View MoreEquity Bank (T) leo imenzidua rasmi akaunti maalum ya utunzani fedha kwa kujiwekea kidogo kidogo ili...
ZaidiEquity Bank (T) imeahidi kuendelea kutoa elimu ya fedha na mikopo nafuu kwa vikundi vya uwekezaji na...
ZaidiCustomers with Equity Bank accounts can now transact seamlessly in any of the Equity Bank branches...
View MoreCustomers will have the freedom to execute forex requirements in real-time in a safe, convenient and...
View MoreEquity Bank Kenya Limited has received two International Standards Certifications - ISO 20000 and...
View MoreEquity Bank Tanzania has announced the appointment of Ms. Isabel Maganga as the new Managing...
View MoreEquity’s Eastern and Central Africa Recovery and Resilience plan is envisaged to provide financing...
View MoreEquity Group has eased its defensive strategy that had been deployed during the economic uncertainty...
View MoreThe partnership will champion the implementation of the Africa Recovery and Resilience Plan which...
View MoreDelegates from the United States of America (USA) have arrived in Dar es Salaam, Tanzania for a...
View MoreEquity Group Holdings Plc today reported Kshs.34.4 billion shillings profit after tax for the nine...
View MoreEQUITY GROUP REPORTS A RECORD KES 46.1B NET PROFIT AND A DIVIDEND PAYOUT OF KES 15.1B
View MoreNairobi Monday 13th May 2024… After reporting a 5% decline in profit after tax for the year ended...
Read MoreNairobi, Kenya, 3rd September 2024: Equity Group unveiled its third annual sustainability report for...
Read MoreNAIROBI, 12th November 2024: Against a backdrop of continued macroeconomic headwinds of high...
Read MoreNAIROBI, 27th March 2025: Equity Group Holdings Plc continues to deliver solid financial results,...
Read MoreNAIROBI, 29th May 2025: Demonstrating strategic agility and resilience in a dynamic global economic...
Read MoreEquity Group Holdings Plc has announced its Q3 2025 results, showcasing a robust performance driven...
Read MoreAsset Loan to Empower Women and Youth Entrepreneurs in Tailoring and Fashion Design Sector
Read MoreMwanza, Tanzania –Tarehe 24 Januari 2026. Benki ya Equity Tanzania, kwa ushirikiano na wadau...
Read MoreBenki ya Equity yazindua “wezesha account” akaunti ya amana ya muda maalum, inayolenga...
Learn More