Equity Bank Tanzania limited imeingia ubia na Klabu ya Simba

Category: Press Release
Published: Friday, 06 November 2020 12:03
Written by Super User
Hits: 130

Equity Bank Tanzania limited imeingia ubia na Klabu ya Simba katika kutoa kadi zenye chapa zao kwapamoja ambazo zinafaida kwa mashirika yote mawili lakini walengwa wakuu ni watakao kuwa wamiliki wa kadi hizo ambao ni wateja/mashabiki na wadau wa mashirika haya mawili kwa umoja wao.

Klabu ya Simba inashauku kubwa kuwapa shabiki/ wadau wake kadi zitakazo warahisishia huduma za malipo mbalimbali, kuweka akiba, kutoa na kuweka hela Benki. Equity Bank dira na dhimaa yake itakuwa Dhahiri kubadilisha maisha ya watanzania kijamii na kiuchumi pia kuongeza idadi ya wanaopata huduma za kibenki nchini.

Akaunti inayompatia shabiki wa Simba kadi ya shabiki (Simba Debit card) pia ina faida zifuatazo;


Kupata kadi hii mtu anastaili kufata utaratibu mzima wa kufungua akaunti ya Benki kwa kutumia kitambulisho cha taifa (NIDA) au namba ya NIDA ama Kitambulisho cha kupiga kura.

Mteja ataitajika kuchangia pesa taslimu zakitanzania Tzs 22,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Simba, ambapo Tzs 10,000/= ni malipo ya kadi na Tzs 12,000 ni ada ya shabiki wa simba kwa mwaka mzima.

Kadi zinazotolewa sasa ni kadi za mashabiki, na siku za usoni kadi za wanachama/wadau zitafuata. Utoaji wa kadi unafanyika kwenye matawi yote ya Equity Bank Tanzania, na sehemu ambapo hakuna tawi la Equity Bank Tanzania mpango mkakati unafanyika na ratiba ya kuzungukia sehemu hizo utatangazwa rasmi.

Tunapenda kukukaribisha kwenye toleo letu jipya la Simba Debit card. Kadi hii inakuja na faida za nyongeza kwa mashabiki na wanachama wa Klabu ya Simba.

Ukiwa na kadi ya Simba Debit Card utafurahia huduma zifuatazo;



Equity Bank Tanzania limited ilianza shughuli zake mwaka 2012 baada ya kuchagua na kuwaelimisha vijana wa kitanzania wapatao 80 nje ya nchi kwa takribani mwaka mmoja. Mpaka sasa, tunayo matawi 15 na mawakala wanaozidi 2,800, huduma ya simu (Eazzy Banking) ambayo inamuwezesha mteja kuendelea na miamala yake popote alipo kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Dira yetu ni kuwa mstari wa mbele katika kuboresha maisha ya kila mwafrika kiuchumi na kijamii. Ni kwa kuzingatia dira hii ambapo tumekuwa tukibuni huduma zinazoendana na soko letu, hali ya maisha ya watu wetu lakini pia kasi ya teknologia duniani na hata wakati mwingine kufikia kuleta huduma ambazo wengi waliomo katika biashara ya utoaji wa huduma za kifedha kuziona kuwa hatarishi.

Equity Bank Tanzania inakaribisha maoni na ushauri ili kuzidi kuboresha huduma zetu kwako. Tutaendelea kujitolea katika kuhakikisha unapata huduma bora.

Asante kwa kuichagua Equity Bank.
*vigezo na masharti kuzingatiwa